EPL: CHELSEA BADO IPO IPO, YATOA SARE NYUMBANI, MAN CTY IKIUA 4 (HIGHLIGHTS + PICs)

Klabu ya Chelsea imeendelea kutokuwa na matokeo ya kuridhisha katika ligi kuu nchini Uingereza. Ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Chelsea imelazimishwa sare na Everton waliokuwa wa kwanza kuzitikisa nyavu za wenyeji kwa mabao ya John Terry aliyejifunga dakika 48 na Mirallas aliyefunga dakika ya 55.


Chelsea walirudi mchezoni kwa goli la Diego Costa la dakika ya 63 aliyetumia vizuri makosa ya Jagielka na Howard. Dakika mbili baadaye Fabregas alipiga shuti lilomgusa beki wa Chelsea na kumpoteza kipa Howard wa Everton.


Dakika ya 90 Everton walipata goli la 3 kupitia kwa Funes Mori kabla ya ya J. Terry kuisawazishia Chelsea Goli 3 dakika ya 90+8.


Matokeo ya mechi zote katika ligi kuu nimekuwekea hapa  chini angalia video za magoli

Chelsea 3 - 3 Everton


Man Cty 4 - 0 C Palace


Newcastle 2 - 1 West Ham



Southampton 3 - 0 West Brom


Bournemouth 3 - 0 Nowrich


Totenham 4 - 1 Sunderland


Aston Vila 1 - 1 Leicester CTY

No comments

Powered by Blogger.