CHELSEA DHOOFU ILHALI YAAMBULIA SARE DAKIKA ZA MWISHO DARAJANI, MAN CITY,SPURS ZAUA

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Chelsea leo iliwabidi kusubiri mpaka dakika za lala salama kuweza kupata sare ya bao 3-3 dhidi ya Everton.




Chelsea ambao wanakamata nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi hiyo walijikuta wakipata mshangao baada ya John Terry Kujifunga kisha Kevin Mirallas kuongeza bao la pili ndipo Diego Costa na Cesc Fabregas walijitahidi na kusawazisha kuufanya mchezo huo kufika dakika ya 90 huku wengi wakiamini kuwa mechi itamalizika kwa sare ya bao 2-2.

Dakika za Nyongeza. Funes Mori alifunga bao la tatu kwa Everton ambalo kila mtu alijua Chelsea wanalala katika mechi hiyo lakini Juhudi binafsi za Nahodha John Terry ziliipatia Chelsea bao la kusawazisha na mchezo kumalizika kwa sare ya bao 3-3.

Manchester City wao wakiwa nyumbani waliifunga Crystal Palace bao 4-0 magoli mawili ya Sergio Aguero huku Phabian Delph na David Silva yalitosha kuwapandisha Man City mpaka juu katika msimamo wakisubiri mechi ya Leicester City.

Katika mechi ya mapema Tottenham wakiwa nyumbani waliinyuka Sunderland bao 4-1

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LEO EPL
Tottenham 4-1 Sunderland
Bournemouth 3-0 Norwich City
Chelsea 3-3 Everton
Man City 4-0 Crystal Palace
Newcastle 2-1 West Ham
Southampton 3-0 West Brom

No comments

Powered by Blogger.