YAMEWAKUTA : LIVERPOOL YAPIGWA 3 UGENINI

Maajabu yanazidi kuendelea kwa timu vigogo katika ligi kuu nchini England baada ya Liverpool kufungwa bao 3-0 na Watford City.



Watford ambao ni wageni katika ligi kuu msimu huu wameibuka na ushindi huo mkubwa katika uwanja wao wa nyumbani na kuwaacha Liverpool midomo wazi.

Makosa ya kipa Wa Liverpool Adam Bodgan kushindwa kuudaka mpira wa kona yalipelekea Watford kupata bao la kwanza likifungwa na mlinzi Nathan Ake huku mshambuliaji Odion Ighalo akifunga mabao mawili.

Kwa matokeo hayo Watford wamepanda mpaka nafasi ya 7 pointi moja tu inawatofautisha na wanaokamata nafasi ya nne Tottenham

No comments

Powered by Blogger.