BARCELONA MABINGWA WA DUNIA

Mabingwa wa Spain Barcelona wameibuka mabingwa wa dunia kwa ngazi ya klabu baada ya kuifunga River Plate ya Argentina kwa bao 3-0 katika mchezo wa fainali huko Osaka Japan.

Messi alitangulia kufunga bao la mapema akitumia pasi ya Neymar  badae  Luis Suarez akafunga mabao mawili kukamilisha ushindi wa bao 3-0.
Barcelona wakiwa na kocha Luis Enrique wameshinda makombe matano kati ya 6 waliyoshindania wakikosa kombe la Mfalme nchini Spain.

Barcelona wamefunga mabao 176 mwaka huu ikiwa ni rekodi mpya ya klabu na wana nafasi ya kuongeza idadi hiyo wakikutana na Real Betis katika ligi.

No comments

Powered by Blogger.