BALE APIGA BAO 4 REAL MADRID IKISHINDA BAO 10
Pambano la ligi kuu ya Spain baina ya Real Madrid na Rayo Valecano limemalizika kwa ushindi wa bao 10-2 walioupata Real Madrid.
Ilikua shoo ya watu watatu Gareth Bale akifunga mabao manne, Benzema akifunga matatu na Ronaldo akifunga mabao mawili huku beki wa timu hiyo Danilo akifunga bao moja kukamilisha ushindi huo mkubwa kwa kocha Raphael Benitez.
Rayo Vallecano walimaliza mchezo huo wakiwa wachezaji 9 baada ya kutolewa wachezaji wake wawili kwa kadi nyekundu. Tito na Raul Baena waliigharimu timu hiyo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu.
Rayo walipata mabao yao mawili mara baada ya Danilo kufunga bao la kwanza kwa Madrid mabao ya Rayo yakifungwa na Antonio Amaya na Jozabed

No comments