UCL : ARSENAL MDOMONI MWA BARCELONA, CHELSEA WARUDISHWA KWA PSG TENA KWA MARA YA TATU


Mechi za Ligi  ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora imepangwa mchana huu huku mabingwa watetezi Barcelona wakipangwa kukutana na Arsenal.Mechi ya kwanza ikipangwa kupigwa Emirates na marudiano kupigwa Nou Camp jijini Barcelona
Chelsea wao wakirudishwa mikononi mwa PSG kama ilivyokua misimu miwili iliyopita katika hatua hii na hii itakua nafasi njema kwa Chelsea kulipiza kisasi baada ya kutolewa awamu zilizopita.
Kikosi cha kocha Rafa Benitez Real Madrid wao wamepangwa kuwakabili AS Roma katika raundi hii mechi ya kwanza ikipigwa nyumbani kwa Roma.
Juventus ambao msimu uliopita walimaliza kama washindi  wa pili watakabiliana na FC Bayern Munich ukiwa ni wasaa muafaka wa kiungo Artudo Vidal kurudi kucheza dhidi ya klabu yake ya zamani yani Juventus.
Manchester City wao wamepangwa kucheza na kikosi kutoka ligi ya Ukraine klabu ya Dynamo Kiev baada ya kumaliza kundi wakishika nafasi ya kwanza mechi ya kwanza Man City wataanzia ugenini
Klabu ya Gent kutoka Ubelgiji ikiweka historia ya kufika michuano hiyo hatua ya 16 bora tangu msimu wa 2000/2001 wakati Anderlecht ilipoingia hatua hiyo watakutana na Wolfsburg ya Ujerumani.
PSV Eindhovein wamepangwa kumenyana na Athletico Madrid wakati Benfica wakicheza na Zenit ya Russia.
Mechi za kwanza zitachezwa Februari 16, 17; 23, 24 na marudiano ni tarehe 8, 9; 15, 16: mwezi March mwaka 2016

No comments

Powered by Blogger.