SERIE A: JUVENTUS YASHINDA, NAPOLI NA ROMA SARE
Mechi za ligi kuu nchini Italia maarufu kama Italian Serie A ziliendelea jana kwa mabingwa watetezi Juventus kuibuka na ushindi huku As Roma na Napoli wakigawana pointi.
Juventus wakiwa nyumbani Juventus Arena waliweza kuwafunga Fiorentina bao 3-1 shukrani kwa magoli ya Juan Cuadrado,Mario Mandzukic na Paulo Dybala katika mchezo ambao ulishuhudiwa na watazamaji 38000 matokeo ambayo yanazidi kuipaisha Juventus ambayo ilianza msimu huu kwa kusuasua.
Jijini Napoli wenyeji Napoli walishindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani Sao Paulo kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana na As Roma katika mechi ambayo watazamaji 36000 waliujaza uwanja huo kushuhudia pambano hilo.
Katika mechi ya mapema hiyo jana AC Milan wakiwa katika uwanja wa nyumbani walienda sare ya bao 1-1 na Helas Verona. Carlos Bacca akitangulia kuipatia AC Milan bao kabla ya Nigel De Jong kutolewa kwa kadi nyekundu na kuwapa Verona penati ambayo ilifungwa na Mkongwe Luca Toni.
Katika mechi zingine Chievo Verona iliifunga Atalanta bao 1-0 wakati Empoli ikiifunga Capri bao 3-1.

No comments