EUROPA LEAGUE : MAN UNITED MTELEMKO YAPANGWA NA TIMU ISIYOJULIKANA, LIVERPOOL WAPELEKWA UJERUMANI

Baada ya kutupwa nje ya makundi katika ligi ya mabingwa barani Ulaya sasa Manchester United wamepangwa kukutana na timu ambayo haijapata jina kubwa katika medani ya soka Midtjylland FC ya Denmark katika harakati za kutaka kubeba ubingwa wa Europa league kwa mara ya kwanza.


Midtjylland ilianzishwa mwaka 1999 baada ya kuungana klabu mbili na kufanikiwa kushinda ubingwa wa Denmark kwa mara ya kwanza msimu uliopita.

Kwa upande wa Liverpool matarajio yao ya kukutana na Borussia Dortmund yamepotea na pengine itakua furaha kwao baada ya kupangwa kukutana na  Augsburg ya Ujerumani timu ambayo ilishangaza wengi msimu uliopita baada ya kumaliza juu ya Dortmund na Schalke 04. 

Tottenham imepangwa kucheza na Fiorentina ya Italia ikiwa ni mwaka mmoja umepita baada ya Tottenham kutupwa nje na timu hiyo ya Italia katika mashindano hayo.

Kikosi cha Gary Neville Valencia wao wamepangwa kukutana na Rapid Vienna, Molde inayofundishwa na Ole Gunnar Solskjaer watakutana na Sevilla wakati Galatasaray watamenyana na Lazio ya Italia.

Mechi nyingine ya kuvutia ni Dortmund watakaocheza na FC Porto mechi ambayo inaangaliwa kama mechi iliyopaswa kuwa ya ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na vikosi vyote kusheheni wachezaji wazuri.

Mabingwa watetezi Villareal wao wamepangwa kucheza na Napoli


Ratiba ya mechi hizo inaonyesha zitachezwa tarehe 18 na marudiano tarehe 25 Februari 2016.


HII NDIYO RATIBA KAMILI



EUROPA LEAGUE LAST 32 DRAW 

  • Valencia vs Rapid Vienna 
  • Fiorentina vs Tottenham
  • Borussia Dortmund vs  Porto
  • Fenerbache vs Lokomotiv Moscow 
  • Anderlecht vs Olympiacos 
  • Midtjylland vs Manchester United
  • Augsburg vs Liverpool 
  • Galatasaray vs Lazio
  • Sparta Prague vs FC Krasnodar 
  • Sion vs Braga 
  • Shakhtar Donetsk vs Schalke
  • Marseille vs Athletic Bilbao 
  • Sevilla vs Molde
  • Sporting vs Bayer Leverkusen
  • Villarreal vs Napoli
  • St Etienne vs Basle 

No comments

Powered by Blogger.