SUAREZ AIPELEKA BARCELONA FAINALI YA KLABU BINGWA YA DUNIA


Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez alifunga mabao matatu peke yake na kuisaidia Barcelona kutinga fainali ya klabu bingwa ya dunia baada ya kuifunga klabu bingwa ya China Guangzhou Evergrande.




Mabingwa hao wa China wanafundishwa na kocha wa zamani wa Brazil na Ureno Luis Felipe Scolari wameipa Barcelona nafasi ya kucheza fainali siku ya Jumapili dhidi ya mabingwa wa America ya Kusini River plate.

Kama Barcelona itashinda kombe hilo itaweka historia ya kuwa timu ya kwanza kuchukua kombe hilo mara 3 baada ya kulichukua mwaka 2009 na 2011

No comments

Powered by Blogger.