SAMWEL ETO'O APEWA "SHAVU" LA KOCHA MCHEZAJI

Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona,Inter Milan,Chelsea na nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto'o ameteuliwa kuwa mchezaji na kocha wa muda wa timu anayoichezea ya huko Uturuki klabu ya Antalyaspor.



Mshambuliaji huyo mwenye miaka 34 ambaye alijiunga na klabu hiyo mwezi Juni kwa mkataba wa miaka mitatu amepewa mechi tatu kuonyesha anaweza kazi hiyo ya ukocha.
Eto'o amechukua nafasi ya kocha Yusuf Simsek ambaye mkataba wake ulisitishwa Disemba 7 mwaka huu.

Antalyaspor watafanya maamuzi ya kumpa Eto'o mkataba wa kudumu baada ya Mwezi Januari.
Eto'o atasaidiwa na Mehmet Ugurlu ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo maamuzi ya kuwa kocha yameshangaza wengi akiwemo pia nyota wa zamani wa Cameroon Patrick M'boma ambaye ameshangazwa na Eto'o kuingia katika nafasi ya ukocha

"Ninachojua hana uzoefu lakini najua atakua kocha mzuri japokua bado kuwa na uhakika" alisema Mboma ambaye alicheza na Eto'o katika timu ya taifa ya Cameroon.

No comments

Powered by Blogger.