BAYERN MUNICH YAWASAINISHA MIKATABA MIPYA NYOTA WAKE WANNE
Wakati majaliwa ya kocha Pep Guadiola ambaye mkataba wake unamalizika mwezi Juni mwakani yakiwa bado hayaeleweki, Bayern Munich imeaamua kuwapa mikataba mipya wachezaji wake wanne.
Xabi Alonso, Javi Martinez,Jerome Boateng na Thomas Muller wote wamesaini mikataba mipya na mabingwa hao wa Ujerumani.
Xabi Alonso, Javi Martinez,Jerome Boateng na Thomas Muller wote wamesaini mikataba mipya na mabingwa hao wa Ujerumani.
Muller mwenye miaka 26 alikua akiwaniwa sana na Luis Van Gaal kwenda kuichezea Man United na kusaini kwake mkataba wake unaomweka Alianz Arena mpaka mwaka 2021 ni dhahiri mshambuliaji huyo ambaye ameitumikia Bayern Munich kwa miaka 15 iliyopita anataka kumalizia soka lake hapo hapo.
Thomas Muller,Jerome Boateng na Javi Martinez wote wamesaini mikataba itakayowaweka mpaka 2021 huku Alonso mwenye miaka 34 akiongeza mkataba wake mpaka mwaka 2017.
No comments