AMEKATWA: CHELSEA YAMTUPIA VIRAGO MOURIHNO

Kocha Jose Mourihno ametimulia kukinoa kikosi cha Chelsea. Mourihno amefukuzwa kazi baada ya kuiwezesha chelsea kushika nafasi y 16 katika msimamo wa Ligi huku ikiwa juu ya msitari wa kushuka daraja kwa pointi 3.


Taarifa kutoka klabu ya Chelsea inasema "Klabu ya Chelsea na Jose Morihno leo tumefikia makubaliano ya kuvunja mkataba kwafaida ya pande zote mbili. Hta hivyo Chelsea itaendelea kumkumbuka Mourihno na inamshukuru kwa mchngo wake mkubwa toka aliporejea mwaka 2013"

Taarifa hiyo inaendelea kusema "Wote tumekubaliana kuwa msimu huu umekuwa mbaya kwa upande wa matokeo na kila mmoja (Chelsea na Mourihno) kukubali kuchukua njia yake ni jambo la muhimu kwetu sote."

"Chelsea inamtaki kila lililojema Jose Mourihno na itaendelea kumheshimu, na kuheshimu kazi aliyoifanya kwa kipindi chote alichoweza kufanya kazi na Klabu hii"

Mourihno atendelea kukumbukwa na Klabu ya Chelsea hasa baada ya kuipa ubingwa wa England mara 3, kombe la FA, Ngao ya Hisani na Kombe la La Ligi.

No comments

Powered by Blogger.