SIMBA NA AZAM HAKUNA MBABE, YANGA YAVUTWA SHATI TANGA.


Pambano la ligi kuu Tanzania bara kati ya mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC na Simba SC limemalizika kwa sare ya bao 2-2



Azam Walitangulia kupata bao la kwanza dakika ya kwanza tu ya mchezo kupitia kwa John Bocco kabla ya Ibrahim Ajib hajaisawazishia Simba na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko matokeo yakiwa bao 1-1.

Kipindi cha pili Simba waliongeza kasi na juhudi pekee za Ibrahim Ajib ziliipa Simba bao la pili akiwatoka mabeki wa Azam na kukwamisha mpira wavuni.

Azam walitulia na kupata bao kupitia tenabkwa nahodha John Bocco baada ya juhudi za Didier Kavumbagu na kufanya mcheso huo kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
Huko Tanga wenyeji Mgambo wameweza kuisimamisha Yanga na kutoka sare ya bila kufungana.

MATOKEO YA MECHI ZA LEO - VPL
Azam FC 2-2 Simba SC
Mgambo 0-0 Yanga
Mwadui 2-0 Stand United
Kagera Sugar 1-1 Ndanda FC
Mbeya City 2-2 Mtibwa Sugar (Mpira unaendelea)

No comments

Powered by Blogger.