NAJUA WAJUA: TIMU HIZI ZITAIPAMBA MICHUANO YA EUROPA LEAGUE MSIMU HUU.



Ni Jumamosi nyingine tunakutana tena katika kipengele hiki cha NAJUA WAJUA katika blog yako ya wapenda soka ambapo leo tutaangalia kwa kifupi juu ya timu 32 ambazo zimebaki katika michuano midogo ya kombe la Europa (Europa League) nani atakutana na nani na msisimko wa michuano hiyo kutokana na kupambwa na timu ambazo ni wababe katika soka la Ulaya


Europa ligi ni michuano ya pili kwa ukubwa katika ngazi ya klabu barani Ulaya na Tofauti na miaka mingine michuano ya mwaka huu itanogeshwa na uwepo wa timu kubwa na maarufu katika soka la Ulaya hapa nazungumzia klabu kama Manchester United,Liverpool, Dortmund, FC Porto n.k

Manchester United klabu inayotajwa miongoni mwa klabu tajiri kabisa duniani ambayo imewahi kuchukua ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya mara 3 imejikuta ikitupwa katika michuano ya Europa League baada ya kushika nafasi ya tatu katika kundi B.

FC Porto, Borussia Dortmund,Bayer Leverkusen na Liverpool ni kati ya timu ambazo ziko katika michuano ya Europa league msimu huu ikumbukwe timu hizi zimeshawahi kunyanyasa katika soka la barani Ulaya na uwepo wao utazidi kutoa hamu ya Wapenda Soka kuikodolea macho michuano hiyo.

Ratiba ya mechi za hatua ya 36 bora itapangwa Jumatatu sambamba na upangaji wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya mabingwa barani humo.

UTARATIBU WA UPANGAJI UTAKUWAJE?

Timu zote zilizofuzu hatua hii zitapangwa katika makundi mawili kundi la Kwanza litakua na timu zilizoongoza makundi ya Europa Leagua pamoja na timu zilizomaliza zikishika nafasi ya 3 katika Klabu bingwa Ulaya ambazo zilipata pointi nyingi.

Kundi la Pili litakua na timu ambazo zilishika nafasi ya pili katika makundi ya Europa League pamoja na timu zilizopata nafasi ya 3 katika makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya ambazo hazikupata pointi nyingi

Timu kutoka kundi la kwanza itacheza na timu yoyote kutoka kundi la pili na hakuna namna timu za kundi moja kukutana katika hatua hii.

Pia timu kutoka katika ligi moja pia haziwezi kukutana katika hatua hii japo katika hatua inayofata swala hili linawezekana.

Na hizi ndizo timu zilizofanikiwa kupenya hatua hii ya 32 bora

KUNDI LA KWANZA 



Athletic Bilbao, FC Basel, Bayer Leverkusen, Braga, FC Krasnodar, Lazio, Liverpool, Lokomotiv Moscow,  Manchester United, Molde FK, Napoli, Olympiakos, 

FC Porto, Rapid Wien, Schalke 04,  Tottenham.

KUNDI LA PILI


Anderlecht, Borussia Dortmund, Fenerbahce, Fiorentina, Galatasaray, Marseille, FC Midtjylland, Partizan Belgrade, Saint Etienne, Sevilla, Shakhtar Donetsk, FC Sion,  Sporting Lisbon, Sparta Prague, Valencia, Villarreal.

NOTE:
 Mechi za Raundi ya 32 bora zitachezwa Februari 18 na marudiano ni Februari 25 mwaka 2016
Kwa leo tuishie hapa na tukutane tena wiki Ijayo katika NAJUA WAJUA NYINGINE

No comments

Powered by Blogger.