REAL MADRID YATOA KICHAPO CHA HATARI, RONALDO NA BENZEMA WAONDOKA NA MIPIRA


Hali inazidi kurudi vyema katika kikosi cha Real Madrid baada ya kutoa kichapo cha bao 8-0 wakiifunga Malmoe FF katika mechi za mwisho ya kundi A katika uwanja wa Santiago Bernabeu.



Ushindi wa leo wa Real Madrid umekuja siku 3 baada ya kutoa kichapo cha bao 4-1 katika ligi kuu nchini Spain.

Magoli manne ya mchezaji bora duniani kwa sasa Cristiano Ronaldo, magoli matatu ya Karim Benzema na moja la Mateo Kovacic yalitosha kuwapa Real Madrid ushindi mkubwa na kujikita kileleni mwa kundi hilo wakiwa na pointi 16 wakifatiwa na PSG wenye pointi 13.

Katika mechi nyingine ya kundi A PSG wakiwa nyumbani waliifunga Shaktar Donetsk bao 2-0 shukrani kwa magoli ya Lucas Moura na Zlatan Ibrahimovic

No comments

Powered by Blogger.