OUT!! MAN UNITED YATOLEWA KWA KICHAPO LIGI YA MABINGWA ULAYA SASA KUCHEZA EUROPA
Matumaini ya mashabiki wa klabu ya Manchester United kusonga mbele katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya mabingwa Ulaya yamezimwa na kichapo cha bao 3-2 walichokipata nchini Ujerumani.
Wakicheza soka safi Wolfsburg walionekana kuutawala mchezo huo wa kundi C na kuwapa United tiketi ya kwenda kushiriki kombe la Europa League.
Antony Martial alitangulia kuipatia United bao la kwanza akiunganisha pasi ya Juan Mata na goli la pili likiwa ni la kujifunga la Beki Joshua Guilavogui huku Wolfsburg wao wakipata magoli yao kupitia kwa Naldo aliyefunga magoli mawili na Vieirinha.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo B PSV Eindhoven wakiwa nyumbani waliifunga CSKA Moscow bao 2-1 na kuifanya klabu hiyo ya Uholanzi kuungana na Wolfsburg kuingia katika hatua ya 16 bora hivyo basi United itawabidi kucheza katika kombe la Europa League.
No comments