MSHAMBULIAJI WA ZAMANI CHELSEA APEWA UKOCHA QPR
Klabu ya Queens Park Rangers imemtangaza mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na kocha wa timu ya daraja la kwanza ya Burton Albion Jimmy Floyd Hasselbaink kama kocha wake mpya.
Hasselbaink mwenye miaka 43 aliiongoza Burton Albion kushinda ubingwa wa ligi daraja la pili nchini England msimu uliopita na sasa amesaini kuifundisha QPR inayopigania kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao.
QPR ilikua chini ya kocha wa muda Neil Warnock baada ya kumtimua Chris Ramsey Novemba 4, mwaka huu.
Hasselbaink alijiunga na Burton mwezi Novemba 2014 na mpaka anaondoka ameiacha klabu hiyo ikiongoza ligi daraja la pili msimu huu ikishinda mechi 33 kati ya 54 tangu alipochukua kazi ya kuifundisha na atajiunga QPR na David Oldfield ambaye alikua kocha msaidizi wakati akiwa Burton.
QPR inakamata nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi ya Championship pointi mbili chini ya mstari wa kucheza hatua ya mtoano kupata nafasi moja kati ya tatu za kupanda daraja.

![]() |
Hasselbaink akiwa na wachezaji wa QPR katika mazoezi ya leo ujumaa |

No comments