MAGUMASHI KAMA BONGO : REAL MADRID YATUPWA NJE KOMBE LA MFALME KWA KUMCHEZESHA ALIYEFUNGIWA
Tumezoea kuona haya yakifanyika Afrika, Lakini hii imetokea ulaya tena kwa klabu kubwa ya mpira wa miguu nchini Hispania.
Real Madrid imejikuta ikitupwa nje ya mashindano ya kombe la mfalme kwa kosa la kumchezesha Denis Cheryshev ambaye alitakiwa kumalizia adhabu yake ya kutokucheza mechi moja, adhabu aliyoipata wakati akiichezea klabu ya Villarreal kwa mkopo msimu uliyopita.
Denis Cheryshev ndiye aliyefunga goli la kwanza. Real Madrid ikishinda ugenini goli 3 dhid ya 1 la Cadiz. Taarifa zinasema kuwa Real Madrid hawakuwa na taarifa juu ya mchezaji huyo kusimamishwa mechi moja na hivyo watakata Rufaa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Hispania na ikishindikana basi wataenda hata Mahakama ya Michezo ya Hispania ili kuhakikisha haki yao haipotei.

No comments