CHICHARITO NDIYE MCHEZAJI BORA KABISA NOVEMBA KATIKA BUNDASLIGA

Javier Hernandez "Chicharito" amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba katika ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga.


Chicharito alijiunga na Bayer Leverkusen akitokea Manchester United ambako alionekana si lolote si chochote kwa kikosi cha kocha Loius Van Gaal kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 7.3 kabla ya kuanza msimu huu wa 2015/2016

Chicharito ambaye pia ni mshambulisji wa timu ya taifa ya Mexico alipelekwa kucheza kwa mkopo katika klabu ya Real Madrid msimu uliopita.

Tangu ajiunge na Bayer Leverkusen Chicharito amefunga magoli 12 katika mechi 17 alizoichezea klabu hiyo ikiwemo magoli 8 katika mechi 6 kwa mwezi Oktoba na Novemba

Bayer Leverkusen wanakamata nafasi ya 6 katika Bundesliga pointi mbili nyuma ya Borussia Monchengladbach ambao wanakamata nafasi ya 4  lakini wako pointi 19 nyuma ya Bayern Munich wanaoongoza.

Chicharito ataiongoza timu yake kucheza kucheza na Barcelona Jumatano katika ligi ya mabingwa Ulaya akiwa ameshafunga magoli manne katika mechi 5 za michuano hiyo msimu huu.

Chicharito mwenye miaka 27 ameichezea Manchester United kwa miaka mitano akifunga magoli 59 katika mechi 157 mechi nyingi akianzia benchi.

No comments

Powered by Blogger.