NAJUA WAJUA: WACHUKUE UBINGWA AU WAINGIE TOP 4 HAKUNA BONASI KWA WACHEZAJI LEICESTER CITY


  • Arsenal wasipoingia Top 4 watakatwa 25% wachezaji
  • Man United wakiingia Top 4 wachezaji kuongezewa 25%



Hakuna kitu kizuri au kibaya kama mkataba na hapa ndipo wenye akili hunufaika na wale wajinga huishia kulalama tu mambo yakiwa sivyo ndivyo mbeleni.

Katika Soka pia hasa klabu za Ulaya mikataba ni kitu ambacho hutiliwa maanani mno na kila msimu mpya unapoanza wachezaji hukaa chini na viongozi kujadili nini wanatarajia kwa msimu mpya hasa katika malipo ya bonusi na malupulupu mengine.

Kwa taarifa yako tu ni kwamba klabu ya LEICESTER CITY ambayo inakamata nafasi ya pili katika msimamo huku ikifanikiwa kukamata usukani wa ligi kuu ya England wiki iliyopita, Wachezaji wake hawataambulia chochote ikiwa timu hiyo itachukua ubingwa au kumaliza ndani ya Timu nne za juu pindi ligi ikimalizika.

Wakati msimu mpya wa ligi kuu nchini England unaanza makubaliano yalikua kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja hivyo hata mikataba yao ilikua watapata kiasi flani iwapo timu haitashuka daraja hivyo kama watamaliza ndani ya Top 4 basi wataambulia pesa kiduchu za kuisaidia timu kutoshuka daraja.

Tofauti na Leicester City klabu zingine zilikua na uhakika wa kuingia Top 4 hata mikataba yao iliakisi hilo na baadhi ya klabu hizo ni

 Arsenal ambao wachezaji wake watakatwa 25%  ya mishahara yao kwa msimu unaofata kama timu hiyo itashindwa kuingia Top 4 na kushindwa kucheza katika ligi ya mabingwa Ulaya.

Manchester United wao kwa upande wao wachezaji watapata ongezeko la mshahara kwa 25% kama watamaliza katika Top 4.

..... Kama ulikua hujui chukua hiyo na tukutane Ijumaa Ijayo katika NAJUA WAJUA

~ Edo DC

No comments

Powered by Blogger.