LEICESTER CITY YARUDI KILELENI, ARSENAL YAZISHUSHA TIMU ZA MANCHESTER
Mambo yanazidi kuwa mazuri kwa Claudio Ranieri baada ya kurudi katika uongozi wa ligi kuu nchini England Leicester City ikiifunga Swansea bao 3-0 kwao.
Alikua kiungo wa kimataifa wa Algeria Riyad Mahrez ambaye alifunga mabao yote matatu na kuifanya klabu hiyo kufikisha pointi 32 na kuongoza ligi kuu nchini England.
Arsenal ikiwa nyumbani iliifunga Sunderland bao 3-1 magoli ya Arsenal yakifungwa na Joel Campbell,Olivier Giroud na Aaron Ramsey huku Giroud akiwazawadia Sunderland bao la kufutia machozi baada ya kujifunga wakati akijaribu kuokoa.
Matokeo hayo yanawafanya Arsenal kupanda mpaka nafasi ya pili ikiwa na pointi 30 ikizishusha Manchester City na Manchester United zenye pointi 29.
Katika mechi ya mapema leo Manchester City walikubali kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa Stoke City huku Man United ikitoka sare ya bila kufungana na West Ham.
MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LEO
- Stoke City 2-0 Man City
- Man United 0-0 West Ham
- Swansea 0-3 Leicester City
- Arsenal 3-1 Sunderland
- Southampton 1-1 Aston Villa
- Watford 2-0 Norwich City
- West Brom 1-1 Tottenham
No comments