KWA TAARIFA YAKO: WAKATI LEO NI MAN UNITED VS CHELSEA, DIEGO COSTA HAJAWAHI KUCHEZA MECHI DHIDI YA MAN UNITED
... Mshambbuliaji wa Chelsea Diego Costa hajawahi kucheza mechi yoyyote dhidi ya Manchester United.
Amekua akitumikia adhabu au mgonjwa kila mara timu yake inapokutana na Manchester United na Jumatatu ya leo wakati Man United watakapoikaribisha Chelsea katika pambano la ligi kuu nchini England kwenye uwanja wa Old Trafford Diego Costa ataikosa tena mechi hii baada ya kupata kadi ya 5 ya njano msimu huu katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Watford ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 2-2.
Man United inakutana na Chelsea katika mechi ambayo mvuto umekosekana baada ya timu hizo kufanya vibaya katika mechi zao katika ligi kuu msimu huu.
No comments