KWA KASI HII YA CHICHARITO VAN GAAL ATAJUTIA KUMUUZA
Goli alilowafunga Barcelona juzi lilikua goli lake la 14 katika mechi 19 tangu ajiunge na Bayer Leverkusen ya Ujerumani pia lilikua bao lake la 5 katika mechi 6 za ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu.
Alijiunga na Bayer Leverkusen akitokea Manchester United ambako alicheza mechi 157 na kufunga magoli 59.
Mashabiki wengi wa United hawakupendezwa na hatua ya kumuuza kijana huyu aliyesajiiwa na Sir Alex Ferguson na kucheza mechi nyingi akianzia katika bench lakini bado alikonga nyoyo za wengi.
Kwa kasi hii ya Chicharito ni dhahiri kocha Louis Van Gaal atakua anajutia kumuuza kijana huyu hasa wakati huu ambapo magoli yamekua magumu kupatikana kwa washambuliaji waliopo United.
No comments