GARY NEVILLE KOCHA MKUU VALENCIA AUNGANA NA MDOGO WAKE PHIL NEVILLE
Mlinzi wa zamani wa Manchester United na England Gary Neville ameteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Valencia inayoshiriki ligi kuu nchini Spain.
Gary Neville, mwenye Miaka 40 ataungana na mdogo wake Phil Neville ambaye tayari alishapata kazi ya ukocha msaidizi wa Valencia wakikumbukia enzi zao wakati wakicheza pamoja katika klabu ya Manchester United huku Gary akiendelea kuwa mmoja wa Makocha wa Timu ya Taifa ya England wakati akiendelea na wadhifa huu mpya huko Spain.
Uteuzi huu wa Neville umekuja kirahisi kwani Mmiliki wa Valencia, Peter Lim, Raia wa Singapore, pia ana Hisa kwenye Klabu ya huko Manchester, Salford City, ambayo pia Neville ni mmoja wa Wamiliki wake.
Neville, ambae mara baada ya uteuzi huu wa huko Valencia amejitoa kuwa mmoja wa Wachambuzi wa TV ya Sky Sports, atatambulishwa rasmi Kesho Alhamisi na Rais wa Valencia Layhoon Chan na katika mechi ya Wikiendi dhidi ya Barcelona ataangalia mechi akiwa jukwaani ila kazi rasmi ataanza Jumatano Ijayo katika mechi dhidi ya Olympic Lyon katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Gary Neville anachukua nafasi ya Nuno Espirito Santo ambae alijiuzulu mara baada ya Jumapili Timu hiyo kufungwa 1-0 na Sevilla kwenye La Liga akiiacha katika nafasi ya 9.

No comments