BARCELONA HATARINI KUWAPOTEZA MESSI NA NEYMAR WANAOWANIWA LIGI KUU ENGLAND
Kumekua na shinikizo kubwa kutoka kwa Manchester City na Manchester United walio tayari kutoa pesa za kuwanunua wakali hao lakini klabu hiyo ambayo ni bingwa wa Ulaya na Spain wanafanya kila liwezekanalo wasiondoke na ili kufanikisha hilo wanatakiwa kuuza hati miliki ya jina la uwanja wao Nou Camp na kupunguza kwa kiwango kikubwa bajeti yao ya usajili ili kupata pesa za kuwabakiza pale Nou Camp.
Licha ya kushinda ubingwa wa ligi ya mabingwa mara tatu katika miaka sita na kupata faida ya paundi milioni 482 msimu uliopita Barcelona bado inakabiliwa na ukata mkubwa mbeleni kwani mishahara pekee ni 73% ya mapato ya klabu kitu ambacho ni kiwango kikubwa zaidi kwa sheria ya matumizi ya pesa michezoni ambayo klabu hiyo imejiwekea.
Mpaka sasa Barcelona haijapata mdhamini wa jezi zake kwa msimu ujao huku kampuni ya Qatar Airways ambao ndiyo wadhamini wa sasa makubaliano ya kuongeza mkataba yakiwa yamesimama baada ya Barcelona kutaka kuongezwa pesa katika mkataba uliopo hivi sasa wa paundi milioni 40 kwa msimu.
Kuwa bingwa mara tatu wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kumeigharimu pia timu hiyo kwani imetakiwa kuwalipa bonasi kubwa wachezaji wake mfano ni
Lionel Messi ambaye hupata nyongeza paundi milioni 2.8 kutoka katika paundi milioni 14.8 anazopata kwa mwaka.
Timu za Manchester zimekua zikiwawania nyota hao na kutokana na uwezo mkubwa wa pesa katika vilabu hivyo na hali inavyoendelea katika klabu ya Barcelona pengine tunaweza kuwaona mmoja kati ya nyota hao akicheza katika moja ya timu hizo kwani Neymar anatakiwa kupewa mkataba mpya na mazungumzo yanaendelea kuuboresha mkataba wa miaka miatano aliousaini mwaka 2013 na siku zote mkataba mpya huambatana na ongezeko la mshahara na posho nyingine.
Klabu za ligi kuu ya England zimekua zikipata mapato mengi kutoka katika wadhamini na hasa haki za matangazo ya biashara tofauti na klabu za Spain.
Mpango wa Barcelona wa kuwanunua Paul Pogba na John Stones utakua mashakani pia baada ya hali inayoendelea hivi sasa na pengine mpango wa kuongeza ukubwa wa uwanja wa Nou Camp kufikia watu 105,000 utasimama pia kama asipopatikana mdhamini.
No comments