LIVERPOOL YAZIDI KUNOGA ILICHOIFANYIA SOUTHAMPTON WE ACHA TU.

Liverpool chini ya kocha mpya Juggen Klopp imeendelea kuimarika baada ya kutoa kichapo kitakatifu cha bao 6-1 kwa 'Watakatifu" Southampton katika dimba la St. Marys nyumbani kwa Southampton.

Mechi hiyo ya Robo fainali ya kombe la Ligi kuu nchini England maarufu kama Capital One limeifanya Liverpool kufika nusu fainali kwa mara ya tatu katika miaka mitano.

Daniel Sturridge alirudi kikosini na kufunga mabao mawili huku Divock Origi akifunga hat-trick (mabao matatu) na lingine moja likifungwa Jordon Ibe ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Sturridge.

Southampton wao walitangulia kupata bao la kuongoza likifungwa na Sadio Mane sekunde ya 39 tu tangu kuanza kwa mpira likiwa ndilo bao la mapema zaidi msimu huu nchini England.

KWA TAARIFA YAKO
  • Divock Origi Alikua hajafunga bao lolote kwa Liverpool na nchi yake tangu kuanza kwa msimu huu
  • Goli la Sadio Mane baada ya sekunde 39 ni la haraka zaidi kufungwa katika mashindano hayo msimu huu.
  • Southampton wamefungwa magoli sita katika mechi ya nyumbani hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1995 walipofungwa 6-2 na Tottenham katika kombe la FA
  • Katika mashuti 7 waliyopiga Liverpool langoni mwa Southampton wamefunga magoli 6.


No comments

Powered by Blogger.