WATFORD VS MANCHESTER UNITED - UCHAMBUZI

Manchester United wanarejea kwenye Ligi Kuu England wakiwa Ugenini na Watford huko Vicarage Road na ushindi kwao utawafanya waongoze Ligi Kuu England.


Ingawa uongozi huo unaweza kuwa ni wa muda tu kwa vile wao ndio wanaanza kucheza hapo Jumamosi Saa 9 Dakika 45 Mchana wakati Timu ya Pili, Arsenal, na Timu ya 3, Leicester City, wanaingia dimbani Saa 12 Jioni huku Vinara Man City wakicheza Saa 2 na Nusu Usiku, lakini kuwa juu kunaweza kuwaathiri kisaikolojia wapinzani wake hao.BPL-TEBO.NOV8B

Mchezaji wa Man United anaeingojea kwa hamu Mechi hii ni Ashley Young ambae alikuzwa Kisoka huko Watford na kuhamia Aston Villa Mwaka 2006 ambao ndio waliomuuza kwa Man United.

Young ameeleza: “Nangojea kwa hamu Mechi hii..huko ndiko nlikoanzia Soka na natarajia kupokewa vizuri…natumai ntapokewa vizuri zaidi kupita Viila. Wengi wa Familia yangu watakuwepo Uwanjani!”

Kuelekea Mechi hii:

Kabla Ligi kusimama kwa Wiki 2 kupisha Mechi za Kimataifa, Man United walikwenda Mechi 7 bila kufungwa na katika Mechi yao ya mwisho Bao za Jesse Lingard, likiwa Bao lake la kwanza kwa Man United, na Penati ya Juan Mata ziliwapa ushindi wa 2-0 dhidi ya West Brom.

Msimu huu, Ugenini, Man United wameshinda Mechi 3, Sare 1 na kufungwa 2 na hivi sasa Man United wapo Nafasi ya 4 kwenye Ligi wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Man City wanaofungana kwa Pointi na Arsenal.

Watford wao wapo Nafasi ya 11 kwenye Ligi baada ya kufungwa 2-1 na Leicester City katika Mechi yao ya mwisho lakini kabla ya hapo walishinda Mechi 2 mfululizo kwa kuzifunga Stoke City Ugenini na West Ham Nyumbani Vicarage Road.

Lakini Watford, chini ya Meneja kutoka Spain, Quique Sanchez Flores, wamekuwa na uhaba wa Magoli, hasa wakiwa Nyumbani, kwa kufunga Bao 3 tu katika Mechi zao 6.

Hali za Wachezaji:

Majeruhi kwa Man United ni Michael Carrick, Antonio Valencia, Anthony Martial, Paddy McNair na Luke Shaw huku Chris Smalling na Marouane wakiwa na maumivu waliyopata kwenye Mechi za Kimataifa ambayo yatatathminiwa kabla ya Mechi.

Majeruhi wa Watford ni Kiungo Jose Manuel Jurado na Beki toka Sweden Joel Ekstrand.

Kumbukumbu:

Watford haijaifunga Man United tangu Ligi Kuu England ianze Mwaka 1992 na mara ya mwisho kukutana huko Vicarage Road, Agosti 2006, Bao za Mikael Silvestre na Ryan Giggs ziliipa ushindi wa 2-1 Man United.

Mtu Denja wa Watford:

Straika kutoka Nigeria, Odion Ighalo, ndie Mfungaji Bora wa Watford ambae ana Goli 7 za Ligi Msimu huu na amezidiwa tu na Straika wa Leicester City, Jamie Vardy, ambae ndie anaongoza kwa Magoli kwenye Ligi Kuu England hivi sasa.

▪▪▪▪ NOTE: Uchambuzi huu umetolewa katika group la Wapenda Soka katika Whatsapp.

No comments

Powered by Blogger.