MAN UNITED YAPATA USHINDI WA JIONI IKO KILELENI

Manchester United ikiwa ugenini iliifunga timu ngeni ya Watford kwa bao 2-1 katika pambano la ligi kuu nchini England lililopigwa katika dimba la Vicarage.


Memphis Depay ambaye alianza kama mshambuliaji wa kati alifunga bao la kwanza la United dakika ya 11 akimalizia pasi ya Ander Herrera ambaye badae alitoka baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Marcos Rojo.

Watford ambao walibadilika sana kipindi cha pili walipata bao zikiwa zimebaki dakika 87 baada ya Rojo kumwangusha mshambuliaji wa Watford Odion Oghalo na nahodha wao Troy Deeney akaukwamisha mpira huo kwa penati.

Wakati Wengi wakiamini mpira huo ungemalizika kwa sare United waliongeza bao la pili baada ya Watford kushindwa kuokoa mpira uliopigwa na Bastian Schwesteiger na Troy Deeney akijifunga.

Kwa matokeo hayo Man United wamefikisha pointi 27 wakiongoza ligi kwa muda hukunwakisubiria mechi zinazoendelea jioni hii.

No comments

Powered by Blogger.