ZANZIBAR HEROES YAANZA KWA KIPIGO CHALLENJI

Mashindano ya mpira wa miguu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) imeaanza leo hii huko Addis Ababa Ethiopia huku ikishuhudia mechi ya Ufunguzi kati ya Burundi dhidi ya Zanzibar Heroes.
????????????????????????????????????

Mchezo huo wa kwanza ulitawaliwa na Burundi iliyokuwa ikiongozwa na Star wa Azam FC Didier Kavumbagu. Juhudi za Burundi kuondoka na Pointi Tatu muhimu zilizaa matunda kunako dakika ya 38 ambapo mshambuliaji wa Burundi Didier Kavumbagu aliandikia Burundi bao la kwanza.

Pamoja na Juhudi za Zanzibar kujaribu kusawazisha bao hilo lakini ilishindikana na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Burundi ilikuwa ikiongoza kwa Bao moja dhidi ya Zanzibar ambao hawakupata kitu.

Kipindi cha pili Zanzibar walijaribu kusawazisha Goli hilo lakini bado mambo yakawa magumu kwao. Dakika 90 ziliisha kwa Zanzibar kukubali kipigo hicho cha bao Moja kwa bila kutoka kwa Burundi.

Ethiopia-cecafa-e1448110702168

Kikosi cha Zanzibar kilikuwa: Mwadini Ali, Nassoro Massoud ‘Chollo’, Mwinyi Hajji, Haidari Issa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mudathir Yahya, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Mateo Anthony, Mcha Khamisi, Awadh Juma Awadh, Ame Ali na Abrahamani Mohammed

Burundi: MacArthur Arakaza, Karim Nizigiyimana, Fataki Kiza, David Nshimirimana, Issa Hakizimana, Yusuf Ndikumana, Fuwadi Ndayisenga, Cedric Amissi, Shashiri Nahimana, Didier Kavumbangu na Laudit Mavugo

No comments

Powered by Blogger.