EL CLASSICO: REAL MADRID VS BARCELONA (VIDEO YA MAGOLI)

Ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga leo imeendelea baada ya mapumziko ya wiki moja kupisha mechi za Kimataifa. Kati ya mechi zilizochezwa leo ni pamoja na mechi inayohusisha miamba ya Hisapania ya Real Madrid na Barcelona maarufu kama El Classico. Mechi imechezwa katika Dimba la Bernabeu, Uwanja wa Nyumbani wa Real Madrid.


Mchezo ulianza kwa kasi na dakika ya 11 tu Luis Suarez aliwanyanyua mashabiki wa Barcelona kwa kufunga goli la kwanza. Wakiwa wanajaribu kutafuta goli la kusawazisha madrid wakajikuta wanamsahau Neymar na kumuacha akifunga goli la pili dakika 39. Mpaka mapumiko goli zilibaki hivyo hvyo Real Madrid 0 - 2 Barcelona.

Barcelona iliingia kipindi cha pili kwa nguvu huku ikitaka kupata goli zingine na kujihakikishia ushindi huo mnono na mnamo dakika ya 53 alikuwa ni Andre Iniesta aliyefunga goli la tatu kwa Barcelona baada ya kugongeana vizuri na Mbrazil Neymar. Dakika ya 75 Luis Suarez akapachika goli la 4 na la mwisho na kufanya mchezo huo kumaliza kwa Real Madrid 0 - 4 Barcelona.

Mchezo huo ulimuacha Barcelona akiongoza ligi kwa tofauti ya pointi 6, unakuwa ni ushindi wa 10 wa Barcelona katika ya michezo 15 waliyocheza na Real Madrid hivi karibuni

Video ya Magoli ya Mchezo huo nimekuwekea hapa My Friend.

No comments

Powered by Blogger.