KILIMANJARO STARS YATOA ONYO KALI CHALENGE, ILICHOIFANYIA SOMALIA MMMH.

Siku chache baada ya kupigwa bao 7-0 na Algeria Watanzania leo wamepata faraja baada ya timu ya taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars kuivurumushia Somalia bao 4-0 katika michuano ya Challenge


Kilimanjaro Stars inayofundishwa na Abdallah Kibadeni ilipata magoli yake manne kupitia kwa Elias Maguli na John Bocco ambao walifunga magoli mawili kila mmoja.
Kilimanjaro Stars iko kundi A pamoja na Ethiopia,Rwanda na Somalia katika michuano inayoendelea huko Ethiopia.

No comments

Powered by Blogger.