HARRY KANE AIPAISHA SPURS KUIBUKA NA USHINDI MNONO DHIDI YA WEST HAM


  • Afunga magoli mawili na kufikisha magoli matano msimu huu
  • Spurs imebakiza pointi mbili kuifikia Arsenal




Magoli mawili ya mshambuliaji Harry Kane yalitosha kuwapa Tottenham Hotspurs ushindi mnono wa bao 4-1 wakiifunga West Ham United katika dimba la White Hart Lane uwanja wa nyumbani wa Tottenham.

Kane alifunga bao moja kila kipindi huku walinzi Kayle Walker na Toby Alderweireld wakifunga bao moja kila mmoja na kuifanya Tottenham kumaliza mchezo wake wa 12 bila kufungwa ikipoteza mchezo mmoja tu wa ufunguzi dhidi ya Man United.

Baada ya mechi hiyo Tottenham sasa wamefikisha jumla ya pointi 24 ikiwa ni pointi 2 nyuma ya Arsenal wanaokamata nafasi ya nne na Harry Kane amefikisha magoli matano katika ligi.

No comments

Powered by Blogger.