INAWEZEKANA BENITEZ NA MKWASA WAMETOFAUTIANA RANGI TU.
Na: Ayoub Hinjo(Ayo's Mata Maestro)
E-mail: hinjo38@gmail.com
Siku huwa hazigandi ni msemo ambao aliutumia msanii wa bongo fleva miaka kadhaa nyuma. Msemo huo unaleta maana kubwa kwenye dunia yetu ambayo kila kukicha inabadilika kutoka na mazingira yanavyokuwa.

Kila Mtanzania alisubiri kwa hamu mechi dhidi ya Algeria, na siku ya mechi ilipowadia kila Mtanzania alikuwa jirani na Tv au wengine walijitokeza uwanjani kutoa sapoti yao kwa timu ya taifa. Lakini mwishowe kila mmoja aliondoka kichwa chini na wengine wakisonya licha ya timu kwenda sare ya 2-2 dhidi ya Algeria, ambao walikuwa kama wamemwagiwa maji pindi walipokuwa nyuma kwa magoli 2-0. Baada ya mechi hiyo hapa nyumbani kilichofuata kule ugenini nchini Algeria ilikuwa historia ya kufungwa magoli 7-0. Mbinu za mchezo na nidhamu ndio vilitufikisha hapo,tumekosa mwelekeo thabiti.
Dunia nzima ilikuwa inasubiri kuona pambano la El Classico ambalo huwa linazikutanisha mahasimu wa jadi nchini Hispania,Real Madrid dhidi ya Barcelona. Hakuna aliye amini kilichoitokea Real Madrid ambayo ilisheheni nyota wao wote wa bei ghali dhidi ya Barcelona ambao wamejengeka kitimu zaidi. Rafael Benitez ni tatizo kwa Real Madrid,mara kadhaa timu imekosa uwiano thabiti hasa pindi inapokutana na timu yenye kasi. Hakuna mtu asiyejua kuwa mzizi wa kushambulia na kuzuia wa timu ya Barcelona upo kwenye kiungo cha timu hiyo lakini Benitez hakujali hilo,alipanga timu kwa kuwafurahisha mabosi na mashabiki ambao walifurika uwanjani hapo. Ni matusi makubwa sana kuwazuia timu ya Barcelona kwa viungo wawili tu kati kati ikiwa wao wameingia na viungo watatu na wanne alikuwa anaibia kucheza kama mshambuliaji.
Modric na Kroos hawakutosha kufanya kazi pale kwenye kiungo labda angeongeza wengine wawili au mmoja wa kushindana na kina Iniesta,Rakitic,Busquet na Alberto. Real Madrid walikosa uwiano kwa kujaza washambuliaji wanne(Ronaldo,Bale,Brnzema,Rodriguez) ambao wote wana uwezo wa kushambulia kuliko kuzuia.
Benitez hakutenda haki kabisa kwa mabosi na mashabiki. Timu imekosa hamasa wala haina hali ya kupambana kikubwa amekosa mbinu mbadala dhidi ya wapinzani.
Inawezekana Benitez na Mkwasa wametofautiana rangi tu ila sehemu zingine wamefanana. Ni mtazamo tu.

No comments