ARSENAL HOI MBELE YA WESTBROM, CHELSEA YAPETA KWA NOWRICH (VIDEO HIGHLIGHTS)

Mashabiki wa Klabu ya Arsenal wameshuhudia timu yao ikiangukia pua mbele ya Westbrom. Mchezo huo uliochezwa katika dimba la Hawthorns huko Westbrom. Arsenal Walijipatia goli la kuongoza kupitia kwa Mshambuliaji wao Oliver Giroud baada ya kupokea mpira wa adhabu kutoka kwa Ozil na kupiga kichwa huku akimuacha kipa wa Westbrom asijue la kufanya

Angalia Highlights ya Westbrom vs arsenal hapa


Goli hilo la Arsenal halikudumu sana kwani Morrison aliweza kusawazisha bao hilo kwa kuunganisha mpira wa adhabu na kuwaacha mabeki wa Arsenal wasijue la kufanya.



Goli la pili la Westbrom lilipatikana kwa  Arteta kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa langoni kwake. Arsenal walikuwa na nafasi ya kusawazisha lakini walishindwa kutumia nafasi hiyo hasa baada ya Santi Carzola kukosa Penati iliyosababishwa na Alex Sanchez.

CHLESEA VS NOWRICH
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya Uingereza ulisuhudia Chelsea akishinda kwa goli moja kwa bila, goli lililofungwa na Diego Costa

Angalia Highlights ya Chelsea vs Nowrich hapa

No comments

Powered by Blogger.