ARSENAL YAPOTEZA, CHELSEA KIDEDEA LEICESTER APAA KILELENI
Arsenal imeshindwa kupata nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi kuu nchini England baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 ugenini dhidi ya West Brom. Oliver Giroud alitangulia kufunga kabla ya Morison kusawazisha na hatimaye Mikel Arteta kujifunga huku Santi Carzola akikosa penati na kuifanya Arsenal kubaki na pointi zao 26 sawa na Man City wanaocheza mechi yao usiku huu.
Chelsea wakiwa nyumbani wameibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 wakiifunga Norwich bao pekee likifungwa na Diego Costa.
Leicester City iliyo katika kiwango bora hivi sasa iliitandika Newacastle bao 3-0 na kupanda mpaka kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na pointi 28 pointi moja juu ya Man United wanaoshika nafasi ya pili.
Matokeo ya mechi zote za ligi kuu England leo

- Watford 1-2 Man United
- Chelsea 1-0 Norwich
- West Brom 2-1 Arsenal
- Newcastle 0-3 Leicester City
- Swansea 2-2 Bournemouth
- Southampton 0-1 Stoke City
- Everton 4-0 Aston Villa
No comments