MAN UNITED, REAL MADRID, JUVENTUS WAAMBULIA SARE. MAN CITY, ATLETICO MADRID MAMBO SAFI ULAYA
Hatua ya tatu ya mechi za makundi ya ligi ya Mabingwa Barani Ulaya imeendelea usiku wa jana kwa mechi nane kupigwa katika viwanja tofauti barani humo.
Mechi kubwa iliyokua ikitazamwa sana ilikua baina ya matajiri wa jiji la Paris klabu ya PSG iliyokua nyumbani ikiwakaribisha Real Madrid kutoka Spain pambano ambalo lilikua kali kwa dakika zote 90 lakini hakuna timu iliyoweza kuziona nyavu za wapinzani na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana
Sambamba na mchezo huo wa kundi A pia kulikua na mchezo mwingine wa kundi hilo Malmo FF Ikiwa nyumbani iliweza kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 Ikiifunga Shakhtar Donetsk ya Ukraine goli la dakika ya Rosenberg dakika ya 17 ya mchezo.
GROUP B
Manchester United ikisafiri mpaka katika jiji la Moscow nchini Russia mahali ambako walibeba ubingwa wa michuano hiyo mwaka 2008 wakiifunga Chelsea kwa mikwaju ya penati ilijikuta ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na wenyeji CSKA Moscow.Iliwabidi vijana hao wa Van Gaal kusubiri mpaka kipindi cha pili kupata bao la kusawazisha likifungwa na Antony Martial akitumia vizuri krosi ya Antonio Valencia. United walifungwa bao la mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa Doumbia aliyemalizia mpira wa penati iliyookolewa na David De Gea
Katika mechi nyingine ya kundi hilo Wolsfburg ilichomoza na ushindi wa bao 2-0 ikiwafunga PSV Eindhoven. Magoli ya Wolsfburg yakifungwa na Bas Dost na Max Kruse
GROUP C
Atletico Madrid wao wakiwa nyumbani waliiadabisha Astana kwa bao 4-0 shukrani kwa magoli ya Saul Niguez,Jackson Martinez, Oliver Torres na Mlinzi wa Astana Dedechko aliyejifunga katika harakati za kuokoa.Galatasaray wakiwa nyumbani waliifunga Benfica bao 2-1 katika mechi nyingine ya kundi hilo
GROUP D
Ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani City of Manchester Stadium (Etihadi) Man City waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 wakiifunga Sevilla ya Spain magoli ya Adil Rami beki huyu wa Sevilla aliyejifunga wakati akiokoa shuti la Wilfried Bonny na bao la dakika za mwisho la Kevin De Bruyne.Mechi nyingine ya kundi hilo iliisha kwa sare ya bila kufungana baina ya Juventus na Borussia Monchengladbach
MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA KWA KIFUPI.
GROUP A
Malmo 1-0 Shakhtar Donestk
PSG 0-0 Real Madrid
GROUP B
CSKA Moscow 1-1 Manchester United
VfL Wolfsburg 2-0 PSV Eindhoven
GROUP C
Atletico Madrid 4-0 FC Astana
Galatasaray 2-1 Benfica
GROUP D
Juventus 0-0 Borussia Monchengladbach
Manchester City 2-1 Sevilla FC
~
No comments