YANGA YAISHUSHIA MVUA YA MAGOLI TOTO AFRIKA, SIMBA YACHAPWA NA PRISONS MBEYA.


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC ya Dar es salaam imeishushia mvua ya magoli Toto Afrika ya Mwanza kwa kuitandika bao 4-1 katika pambano la ligi kuu Tanzania bara katika uwanja wa Taifa Jijini Dar.

Goli la mapema la beki wa Yanga Juma Abdul akipiga shuti la umbali wa mita 25 lilitosha kuwapa Yanga uongozi wa bao 1-0 mpaka mapumziko huku Donald Ngoma wa Yanga akishindwa kufunga penati baada ya shuti hafifu alilopiga kuokolewa na kipa wa Toto Afrika.

Kipindi cha pili Yanga walibadilika na kuongeza mashambulizi langoni mwa Toto Afrika huku Simon Msuva aliyeingia kipindi hicho akiwa chachu ya ushindi baada ya kufunga magoli mawili huku akisaidia kupatikana bao moja lililofungwa na Amiss Tambwe.

Kwa matokeo hayo Yanga wanafikisha pointi 19 katika uongozi wa ligi hiyo wakisubiri pambano kati ya Ndanda FC watakaowakaribisha Azam FC kesho.

PRISONS 1-0 SIMBA SC

Wakati huo huo Jijini Mbeya Mnyama Simba alikubali kulambishwa mchanga na kuchapwa bao 1-0 na maafande wa Tanzania Prisons pambano lililopigwa katika dimba la Sokoine jijini humo.

STAND UNITED 3-0 MAJIMAJI FC

Mshambuliaji Elias Maguri amezidi kuwaonyesha Simba kuwa walikosea kumwacha baada ya kuifungia timu yake mabao mawili kati ya matatu waliyoyafunga dhidi ya Majimaji huku Pastory Athanas akifunga bao moja katika mchezo huo uliovurumishwa katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga.


COASTAL UNION 1-0 KAGERA SUGAR 

Jijini Tanga baada ya Coastal kumtimua kocha wao leo wameweza kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.

No comments

Powered by Blogger.