CHICHARITO AIPANDISHA BAYER LEVERKUSEN KIMAUZO NA UMAARUFU
Wakati Manchester United wakimwona hafai na kuamua kumuuza klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani imenufaika kwa hali ya juu kutokana na kumnunua mshambuliaji raia wa Mexico Javier "Chicharito" Hernandez
Klabu hiyo ya Ujerumani imejizolewa mashabiki lukuki kupitia mitandao ya jamii tangu ilipotangaza usajili wa Chicharito mtu ambaye inaaminika kuwa anapendwa sana na mashabiki kila timu anayoichezea tangu alipokua Chivas, Man United, Real Madrid na sasa Bayr Leverkusen.
Matangazo ya kuuzwa jezi ya Chicharito katika mtandao wa klabu iliifanya "server" ya klabu hiyo kushindwa kuendelea baada ya watu wengi kuingia na kuomba kununua jezi hiyo
Matangazo ya kuuzwa jezi ya Chicharito katika mtandao wa klabu iliifanya "server" ya klabu hiyo kushindwa kuendelea baada ya watu wengi kuingia na kuomba kununua jezi hiyo
Katika mtandao wa twitter wa akaunti ya Bayer Leverkusen habari ya Chicharito baada ya kuandikwa iliweza kurudiwa na watu 15,000 (retweets) idadi ambayo haijawahi kutokea katika historia ya klabu hiyo.
Katika mtandao wa Facebook baada ya tangazo la kusajiliwa Chicharito tangazo hilo lilipata likes 50,000 siku hiyo hiyo ya kwanza ikiwa pia ni rekodi ya klabu.
Chicharito mwenyewe ana mashabiki milioni 8 katika mitandao ya jamii milioni 5.64 wakiwa katika mtandao wa twitter idadi ambayo ni ni mara mbili ya klabu kubwa kabisa Ujerumani Bayern Munich na zaidi ya mara mbili ya akaunti za twitter za Bundesliga zote kwa pamoja yani ile ya Kiingereza na ile ya Kijerumani. Liverkusen wao wana mashabiki 170,000 tu katika twitter.
Mashabiki wengi wa Chicharito wameandika katika mitandao ya jamii kwamba wanaanza kuifatilia Bayer Leverkusen kwasababu ya uwepo wa Chicharito huko hatua ambayo itaongeza mauzo ya bidhaa za timu hiyo ya Bundesliga ambayo leo itacheza dhidi ya Darmstadt mechi itakayoanza majira ya saa 10 na nusu.
No comments