ROONEY KUIKOSA LIVERPOOL LEO FELLAIN KUONGOZA MASHAMBULIZI


Kikosi cha kocha Louis van Gaal leo kinaweza kumkosa nahodha na mshambuliaji Wayne Rooney ambaye amepata maumivu ya misuli ya paja na atahitaji kupatiwa vipimo vya mwisho leo kuona kama ataweza kucheza.

Kama Rooney atakosekana  basi Kuna kila dalili Marouane Fellaini ataanza kama mshambuliaji huku Ander Herrera akianza kama namba 10 yani akicheza nyuma ya mshambuliaji na hii ni kutokana na ugeni wa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Antony Martial huku Adnan Januzaj akipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Borussia Dortmund.

Kikosi cha Manchester United jana kiliwasili katika hoteli Lowry jijini Manchester tayari kwa pambano dhidi ya Liverpool leo jioni akiwemo David De Gea ambaye jana alisaini mkataba mpya.

Martial akiwasili na McNair

De Gea akipungia mashabiki wakati anaingia hotelini

LVG akipiga selfie na mashabiki jana




Wayne Rooney delivers emotional speech after goal record

No comments

Powered by Blogger.