DE GEA AWEKA SILAHA CHINI NA KUSAINI MKATABA MPYA MAN UNITED


Kipa namba moja wa Man United ameamua kuweka "Silaha" chini na kusaini mkataba mpya wa miaka minne kukipiga katika klabu hiyo ya Old Trafford.

De Gea mwenye miaka 24 almanusura ajiunge na Real Madrid baada ya uhamisho huo kukwama siku ya mwisho ya usajili kwa kuchelewa karatasi za usajili kitu ambacho kiliwauzi Real Madrid lakini ilikua ni faraja kwa Mashabiki wa United kutokana na umahiri wa kipa huyo

De Gea alijiunga na United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 18.9 na ameshachezea United mechi 175. 

No comments

Powered by Blogger.