KIUNGO MCHEZESHAJI AIKIMBIA CHELSEA
Mchezaji aliyelelewa na Chelsea Josh McEachran amekamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya daraja la kwanza (Championship) ya Brentford FC kwa uhamisho ambao haujawekwa wazi.
Josh mwenye miaka 22 ameshaichezea Chelsea mechi 22 huku 11 kati ya hizo ikiwa katika Ligi kuu nchini England na 6 ni katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Mchezaji huyo ambaye ana uwezo wa kucheza namba nyingi ikiwemo kiungo mkabaji na kiungo mchezeshaji ametambulishwa leo na klabu yake hiyo mpya.
Katika mtandao wao wa Twitter Brentford FC wameandika Josh amesaini mkataba wa miaka minne.
No comments