HAMISI KIIZA ATUA KIVINGNE VPL
Simba Sports club inaendelea na mkakati wa kuboresha timu kwa ajili ya msimu wa mwaka 2015 – 2016. Baada ya kuboresha benchi la ufundi kwa kupata kocha mpya, kocha wa viungo na kocha wa magolikipa, Simba Sports Club imegeukia uboreshaji wa timu yake.
Simba imemsajili Hamis Kiiza Raia wa Uganda kuja kuongeza Nguvu kwenye team hiyo na kushirikiana na Mganda mwenzake Emmanuel okwi.
Hamis kiiza maarufu (Diego) atafika nchini siku ya Alhamisi tarehe 2 July 2015 kwa ajili ya kufanya vipimo. Ikiwa atafanikiwa vipimo basi utaratibu wa usajili utaendelea.
Hamis Kiiza ni mchezaji kutoka Uganda ambaye pia anacheza timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes.
Wakati huo huo inasemekana kuna beki Raia wa burundi tayari yupo katika hatua ya mwisho kujiunga na team hiyo ya Simba sports club.
Simba mpaka sasa inakuwa na wachezaji watano wa kigeni, wanne wakiwa Waganda, beki Juuko Murushid, washambuliaji Simon Sserunkuma Hamis kiiza Diego na Emmanuel Okwi.
No comments