MESSI AKARIBIA KUCHUKUA UBINGWA NA AGENTINA.


Kile kitendawili cha lini Messi ataisaidia timu yake ya taifa kinaelekea kuteguliwa baada ya Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Argentina kuiongoza nchi yake kutinga katika fainali za kombe la mataifa ya Amerika Kusini Copa America.
Messi ambaye ameshashinda makombe yote ngazi ya klabu amiwa na Barcelona akishinda pia tuzo ya mwanasoka bora wa dunia mara 4 mfululizo hajawahi kushinda kombe akiwa na timu yake ya taifa hivyo kupata nafasi nyingine ya kutaka kuwaonyesha watu kama yeye ni mkali hata timu yaTaifa.

Argentina usiku wa kuamkia leo imeibuka na ushindi wa bao 6-1 wakiifunga Paraguay katika mechi kali ya nusu fainali ya pili iliyopigwa katika dimba la Municipal Alcaldesa Ester Roa Mjini Rebolledo Nchini Chile. Lionel Messi akitengeneza pasi za magoli mawili ya mwanzo yaliyofungwa na Marcos Rojo na Javier Pastore huku Paraguay wakipata bao moja kupitia kwa Lucas Barrios.
Kipindi cha pili kilikua kibaya zaidi kwa Paraguay na kukubali mabao mengine manne Angel Di Maria akifunga mara mbili, Gonzalo Higuain na Sergio Kun Aguero wakifunga mara moja moja.
Kwa matokeo hayo sasa Argentina watacheza fainali na wenyeji Chile ambao walitinga Fainali baada ya kuichapa Peru bao 2-1.
VIKOSI:
ARGENTINA (Mfumo 4-3-3): 
Romero; Zabaleta, Otamendi, Demichelis, Rojo; Mascherano, Biglia, Pastore; Messi, Di Maria, Aguero.
Akiba: Casco, Banega, Lamela, Gago, Marchesin, Higuain,Tevez, Lavezzi, Guzman, Roncaglia, Pereyra.

PARAGUAY (Mfumo 4-4-2): 
Villar; Aguilar, da Silva, B.Valdez, Piris; D.Gonzalez, Caceres, Ortiz, Benitez; N. Valdez, Santa Cruz.
Akiba: 
Barrios, Bobadilla, Aranda, M. Caceres, Silva, Balbuena, Romero, Molinas, Ortigoza, A. Aguilar, Samudio, Martinez.

No comments

Powered by Blogger.