KABLA HUJALALA KAMATA HIZI TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA
Manchester United wanamtaka mshambuliaji wa Atletico Madrid, Mario Mandzukic, 29, mwaka mmoja tu baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Spain akitokea Bayern Munich kwa pauni milioni 18.5 (Sun),
United pia wanamtaka beki wa kulia wa Paris St Germain Gregory van der Wiel, 27, baada ya Dani Alves kuamua kubakia Nou Camp (Mail),
Louis van Gaal pia anafikiria kumfuatilia beki wa kulia wa Southampton Nathaniel Clyne, 24 (Express),
meneja mpya wa West Ham Slaven Bilic amekabidhiwa fungu la kutosha la kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy, 28, na kiungo wa Barcelona Alen Halilovic, 18 (Guardian),
usajili wa kwanza chini ya Bilic utakuwa kiungo kutoka Sampdoria Pedro Obiang, 23, kwa pauni milioni 4.4 (Mail),
meneja mpya wa Derby County Paul Clement anataka kumsajili mshambuliaji wa Hull City Tom Ince, 23, kwa pauni milioni 6 (Mirror),
meneja wa Everton Roberto Martinez anataka kumsajili beki wa Crystal Palace Scott Dann, 28 (Independent),
kiungo wa Paris St-Germain Yohan Cabaye, 29, anafikiria kujiunga na Crystal Palace (Le Parisien),
meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anamtaka mshambuliaji Timo Werner, 19 kutoka Stuttgart (Mirror),
mshambuliaji wa Manchester City Alvaro Negredo, 29 atasaini kwenda Valencia kwa mkataba wa kudumu (Manchester Evening News),
Manchester City wapo tayari kumuuza Edin Dzeko, 29, lakini wanataka pauni milioni 20. Liverpool hawamtaki tena Dzeko lakini Jose Mourinho anafurahishwa na mchezaji huyo (Daily Mail),
Arsene Wenger anamfuatilia kipa wa Real Madrid, Iker Casillas. Wenger angependa kumchukua Petr Cech, lakini atamchukua Casillas iwapo atataka kuondoka Bernabeu (Evening Standard),
Real Madrid wanataka kumsajili kipa wa Espanyol, Kiko Casilla, kuwa kipa msaidizi wa David De Gea (Daily Mirror),
PSG watatazama uwezekano wa kuziba pengo la Zlatan Ibrahimovic kwa kumchukua Ronaldo msimu ujao baada ya huu mpya (Daily Mirror),
Juventus wapo tayari kutoa pauni milioni 30 kumsajili Oscar kutoka Chelsea, ili kuziba nafasi ya Andre Pirlo (The Sun),
PSG hawatomuuza Marco Verratti msimu huu licha ya kunyatiwa na Arsenal, Manchester United na Real Madrid (Daily Express),
Atletico Madrid wanakaribia kumsajili mshabuliaji wa Villareal Luciano Vietto (AS),
kipa wa Chelsea Petr Cech anataka kwenda Arsenal. PSG walikuwa wakimtaka, lakini wamejitoa kwa sababu Cech anataka kubakia London (The Independent),
na AC Milan wamejiunga katika mbio za kumsajili beki wa Atletico Madrid Miranda ambaye anasakwa pia na Chelsea na Manchester United (Daily Star).
No comments