HABARI KALI ZA SOKA ASUBUHI HII
■ Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda jana alifungua michezo ya umoja wa Shule za Sekondari Tanzania UMISETA katika jiji la Mwanza na kuwaasa vijana kujituma ili waweze kuiwakilisha Tanzania.
■ Mechi ya kimataifa ya soka kati ya Marekani na wenyeji Ujerumani ambao ni mabingwa wa Dunia ilimalizika kwa Ujerumani kukubali kichapo cha bao 2-1 katika mchezo mkali ambao ulishuhudiwa Marekani wakitumia vijana wengi ambao ni chipukizi katika soka.
■ Kocha na mchezaji wa zamani wa Brazil Zico ameweka wazi kuwa anataka kuwania nafasi ya kuwa Rais wa shirikisho la dunia FIFA baada ya Sep Blatter kujiuzulu kutokana na sakata la Rushwa linalofurukuta katika shirikisho hilo.
■ Klabu ya Swansea City ya England imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana Andrew Ayew toka mabingwa wa zamani wa Ulaya Olympic Marseille bila ada yoyote ya uhamisho baada ya mkataba wake kumalizika na amesaini mkataba wa miaka minne kuichezea klabu hiyo inayotumia uwanja wa Liberty.
■ Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ameendelea na mpango mkakati wa kumsajili mshambuliaji nyota wa Mabingwa wa Italia Juventus Carlos Tevez.
■ Baada ya miaka 9 ya kuichezea Arsenal akiandamwa na majeruhi kibao ambayo yalimweka nje kwa kipindi kirefu kiungo mfaransa Abou Diaby ameambiwa hatapewa mkataba mwingine na klabu yake ya Arsenal hivyo kumfanya kuwa mchezaji baada ya Julai Mosi.
■ Kocha wa zamani wa England Steve McLaren ameteuliwa kuinoa Newcastle United kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya timu hiyo kuwa katika mchakato wa kumtafuta kocha baada ya kuondoka kwa Allan Pawdew.
■ Beki wa Barcelona Dani Alves amefunguka na kusema kuwa Lionel Messi ndiye aliyemshawishi kubaki na kusaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Ulaya mkataba wa miaka miwili ambao utamweka Catalunya mpaka mwaka 2017.
■ Bayern Munich wameanza mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Senegal anayekipiga katika klabu ya Southampton Sadio Manne ambaye amekua mhimili mkuu katika safu ya ushambuliaji ya wakali hao ambao walikua na msimu mzuri sana ambao umemalizika.
No comments