SAFARI YA PEP GUADIOLA KUIANGAMIZA "FAMILIA YAKE" INAANZA LEO.
Mechi ya pili ya nusu Fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya itachezwa leo kati ya Wenyeji Barcelona watakaomkaribisha Pep Guadiola na Bayern Munich yake katika dimba la Camp Nou mjini Catalunya Barcelona Hispania.
Pep Guadiola ndiye kocha aliyetoa mchango mkubwa katika kuitengeneza Barcelona iliyotikisa dunia miaka michache iliyopita ikicheza soka safi na kubeba makombe 14 ndani ya miaka minne tu tena makombe makubwa kabisa katika ngazi ya klabu.
Atarudi Catalunya leo ni kama kuiangamiza familia aliyoitengeneza kwa mafanikio lakini wakati huu akiwa na kikosi cha Bayern Munich anachojaribu kukitengeneza hivi sasa.
Mechi hii ni ya kwanza baina ya timu hizo katika hatua hii ya nusu fainali na marudiano yake yatakua wiki ijayo Jijini Munich Ujerumani.
Bayern Munich wataingia katika mechi ya leo wakiwa na majeruhi lukuki tofauti na Barcelona ambao mlinzi wao Jeremy Methieu pekee ndo ataukosa mchezo wa leo.
Bayern Munich watakua bila ya Arjen Robben, Franck Ribery, David Alaba na Holger Badstuber ambao ni majeruhi wakati Roberto Lewandowski yeye anaweza kucheza akiwa na kifaa maalumu usoni kuzuia kuumia baada ya kuvunjika pua walipocheza na Dortmund katika kombe la Ligi nchi Ujerumani.
Lionel Messi anatarajia kufikisha mechi yake ya 100 leo akiwa na Barcelona katika michuano ya Ulaya lakini Thiago Alcantara ambaye aliihama Barcelona kwa kukosa nafasi atarudi dimbani kukutana na kaka yake Rafinha ambaye bado anakipiga Barcelona.
Barcelona leo watataka kulipa kisasi cha kufungwa na Bayern Munich uahindi wa jumla wa bao 7-0 katika michuano hiyo mwaka 2013. Ikiwa inazidi kujijenga kiuwezo na uchezaji kwasasa ikiwa na utatu unaotisha katika kupachika mabao Lionel Messi,Luis Suarez na Neymar ambao kwa pamoja wameshafunga mabao 108 na kutoa pasi za magoli 50 msimu huu huku Barca ikishinda bao 16 katika mechi mbili zilizopita katika ligi kuu.
Kitu pekee wanachojivunia Bayern Munich leo ni kuwa na kocha ambaye anaifahamu Barcelona nje ndani ambaye atawapa mwongozo wa nini wanatakiwa kukifanya ili kushinda mengineyo yatabaki kwa wachezaji wenyewe.
Itakua mechi ambayo marafiki wawili watakutana tena na safari hii wakiwa ni makocha Pep Guadiola na Jose Henrique ambao wamewahi kucheza pamoja katika kikosi cha Barcelona
BAYERN MUNICH CHINI YA PEP GUARDIOLA MSIMU HUU
Wamecheza mechi : 47
Wameshinda: 35
Wakitoka sare : 5
Wakifungwa : 7
Wamefunga magoli: 117
Imefungwa magoli: 28
Imeshinda kombe 1: Bundesliga
Bado inapigania: Champions League (nusu fainali)
BARCELONA CHINI YA LUIS ENRIQUE MSIMU HUU
Wamecheza mechi : 53
Wameshinda: 45
Wakitoka sare : 3
Wakifungwa : 5
Wamefunga magoli: 159
Imefungwa magoli: 28
Kombe Ililoshinda : hakuna
Bado inapigania: La Liga (Nafasi ya kwanza), Copa del Rey (Fainali) Ligi ya Mabingwa Ulaya (Nusu Fainali)
Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo.
No comments