MESSI HATARI APIGA MAWILI NA KUSAIDIA MOJA


Magoli mawili ya Lionel Messi na moja la Neymar yalitosha kuwaweka Barcelona katika nafasi nzuri ya kufuzu kucheza fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu.

Barcelona waliibuka na ushindi huo wa bao 3-0 wakiwafunga Bayern Munich katika mechi ya nusu fainali ya kwanza iliyopigwa katika dimba la Nou Camp jijini Barcelona Spain.

Alikua mshambuliaji Lionel Messi ambaye alifunga magoli mawili na kusaidia kupatikana goli la tatu na kumfanya kufikisha magoli 77 katika historia ya michuano hiyo na kuwa ndiye mfungaji bora kabisa kuwahi kutokea akimpita Cristiano Ronaldo mwenye magoli 76.

Mtihani walionao Bayern Munich ni mkubwa mno kuweza kuvuka hatua hii kwani wanatakiwa kushinda si chini ya bao 4 kitu ambacho ni kigumu kukifikiria kutokana na ubora wa Barcelona ya sasa.

Neymar,Messi n Suarez wamefikisha magoli 111 msimu huu na kuwafanya Barcelona kuongoza katika timu zilizofunga magoli mengi zaidi msimu huu barani Ulaya.

WAFUNGAJI BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA

  1. Lionel Messi (Mechi 96) - 77
  2. Cristiano Ronaldo (Mechi 113) - 76
  3. Raul Gonzalez (Mechi 142) - 71
  4. Ruud Van Nilsteroy (Mechi 73) - 56
  5. Thiery Henry (Mechi 112) - 56

No comments

Powered by Blogger.