ADEBAYOR AIBUA MAMBO MAZITO KUHUSU FAMILIA YAKE
Emmanuel Adebayor ameamua kuanika mambo yote ambayo ameyapitia na familia yake na hiki ndicho alichokisema
"Nimejaribu kufika historia hii kwa kipindi kirefu lakini kwa sasa nimeamua niweke wazi kile kilichotokea kati yangu na familia yangu. Najua kwamba mambo ya kifamilia yanatakiwa kujadiliwa kifamilia na si wazi lakini nafanya hivi ili watu wengine wajue nini kilitokea katika kipindi chote hicho. Naomba mjue kwamba hakuna chochote katika haya yahusuyo fedha.
Nilipokuwa na miaka 17, kipindi nilichoanza kulipwa mshahara wangu wa kwanza kama mchezaji wa mpira, niliijengea nyumba familia yangu na kuhakikisha kwamba wapo salama. Kama mnavyojua nilikuwa mchezaji bora wa Afrika mwaka 2008. Pia nilimnunulia mama nyumba kama shukrani kwa kila kitu alichonifanyia.
Katika mwakahuohuo, nilimleta Uingereza ili afanyiwe uchunguzi wa mwili wake wote kwa undani zaidi na kupewa dawa zenye nguvu kwa ajili ya afya yake. Wakati binti yangu anazaliwa, nilimpigia mama simu ili kumpa taarifa lakini akanikatia simu na hakutaka kunisikiliza.
Baada ya kusoma komenti za watu wengi, walisema kwamba mama alitakiwa kumuona mchungaji TB Jishua. Mwaka 2013, nilimpatia mama kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kwenda kumuona mchungaji huyo nchini Nigeria.
Alitakiwa kukaa huko kwa wiki moja, lakini siku mbili baada ya kukaa huko, nilipigiwa simu na kuambiwa kwamba aliondoka. Mbali na hivyo, nilimpatia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuendeleza biashara yake ya mghahawa, pia na kufungua biashara nyingine. Sikuishia hapo, niliwaruhusu watumie jina langu, picha yangu ukutani katika mghahawa huo ili kuwavutia watu wengi zaidi. Je, ni kitu gani kingine mtoto anaweza kukifanya kuisapoti familia yake?
Miaka miwili iliyopita nilinunua nyuma kule Lagon, nchini Ghana kwa kiasi cha paundi milioni 1.2 (Zaidi ya shilingi bilioni 1.). Nilijisikia huru kumwambia dada yangu mkubwa, Yabo Adebayor aende akaishi katika nyumba hiyo.
Pia nikamruhusu mdogo wangu Daniel akakae katika nyumba hiyohiyo. Miezi michache baadae, nilikuwa kwenye likizo hivyo nikaamua kwenda kwenye ile nyumba. Nilipatwa na mshtuko baada ya kuona magari mengi yakiwa yamepakiwa. Dada yangu aliamua kuipangisha nyumba ile pasipo kunitaarifu, pia alimfukuza mdogo wetu Daniel kwenye nyumba ile.
Kumbuka kwamba nyumba ilikuwa na vyumba 15. Nilipomuita na kumuuliza ili anielezee, alichukua dakika 30 kunitukana simuni. Nikaamua kumpigia mama ili ajaribu kunielezea lakini naye akafanya hivyohivyo, akanitukana. Dada huyohuyo ndiye aliyesema kwamba sina shukrani.
Kaka yangu Kola Adebayor yupo Ujerumani kwa miaka 25. Alikwenda nyumbani mara nne tena kwa gharama zangu. Pia ninagharamia gharama ya elimu ya watoto wake. Nilipokuwa Monaco, alikuja na kuhitaji fedha kwa ajili ya kufanya biashara. Mungu pekee ndiye anayejua nilimgawia kiasi gani. Sasa hiyo biashara ipo wapi?
Wakati ndugu yetu Peter alipofariki, nilimtumia Kola kiasi kikubwa cha fedha ili aweze kwenda nyumbani. Hakwenda kwenye mazishi. Na leo hii, huyohuyo Kola anasema kwamba nilihusika katika kifo cha Peter. Kivipi?
Ndiye mtu huyohuyo aliyekwenda kuwaambia waandishi wa habari wa The Sun ili apate fedha. Pia, (The Sun) wakamtuma barua katika Klabu niliyokuwepo ya Real Madrid ili nifukuzwe.
Nilipokuwa Monaco niliona ni vizuri familia yetu ikawa ya wachezaji wa mpira. Nilichokifanya ni kuhakikisha kwamba mdogo wangu Rotimi anaanza mpira kwenye akademi kule Ufaransa. Miezi michache baadae, mbali na wachezaji 27, aliiba simu za wachezaji 21.
Siwezi kuzungumza mengine kuhusu Peter kwa kuwa hatunaye kwa sasa, Mungu amlaze mahali pema peponi.
Dada yangu Lucia bado anawaambia watu kwamba baba aliniambia nimpeleke Ulaya. Lakini kulikuwa na umuhimu gani wa kwenda Ulaya? Kila mtu aliyekuwa Ulaya, yupo kwa sababu fulani.
Nilikuwa nchini Ghana wakati nilipopokea taarifa kwamba mdogo wangu, Peter alikuwa mgonjwa mno. Nikaendesha gari kwa kasi ili niwahi kumuona na kumsaidia. Nilipofika, mama akaniambia siwezi kumuona hivyo nimpe fedha yeye atakamilisha kila kitu.
Ni Mungu pekee ndiye anayejua nilimfawia kiasi gani siku hiyo. Watu wanasema sikufanya juhudi zozote kuokoa maisha ya mdogo wangu, Peter. Hivi mimi ni kichaa kusafiri kwa masaa mawili, tena kwa haraka kuwahi nyumbani kisha nisifanye lolote?
Mwaka 2005 nikaitisha kikao ili tumalize matatizo ya kifamilia. Nilipowauliza kuhusu mawazo yao wakaniambia kwamba kila mtu nimjengee nyumba na niwalipe mishahara kila mwezi. Leo nipo hai, tayari wamekwishatumia vyote nilivyokuwa navyo, vipi nikifa?
Kwa sababu hizo zote, ilichukua muda mrefu kuweka misingi imara huku Afrika. Mara kwa mara najitahidi kuwasaidia watu walio na uhitaji, wanatakiwa kuniuliza kama nikifanyacho ni kibaya.
Ninapoandika hili si kwamba ninataka kuiteta familia yangu bali ni kuwafundisha Waafrika wengine kujifunza kupitia haya".
Alimaliza kusema Adebayor ambaye anaichezea Tottenham hivi sasa.
No comments