MAN UNITED HALI MBAYA YAPOTEZA MECHI YA TATU MFULULIZO
Manchester United imepoteza mchezo wa tatu mfululizo katika ligi kuu ya England leo kwa kukubali kufungwa bao 1-0 na West Bromwich Albion pambano lililopigwa katika dimba la Old Trafford.
Manchester United ambao walitawala mchezo huo kwa kupiga pasi nyingi na kumiliki asilimia kubwa ya mchezo huo ilishindwa kabisa kugeuza ubao wa matokeo.
Goli pekee la West Brom lilipatikana kwa njia ya adhabu ndogo karibu kabisa na mstari wa boksi likifungwa kwa ufundi na Jonas Olson ambaye aliugusa mpira uliopigwa na Chris Brunt dakika ya 64 ya mchezo.
Man United itabidi wajilaumu wenyewe kwani Robin Van Perse alikosa penati ambayo ingeweza kuwarudisha Man United na pengine wangeweza kuibuka na ushindi baada ya kipa wa West Brom kudaka penati hiyo iliyotokana na mpira ulioshikwa na mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino katika eneo la hatari.
Matokeo hayo yanazidi kuiondoa United katika nafasi ya kushika nafasi ya pili katka msimamo ligi itakapomalizika na inabaki na pointi 65 katika nafasi ya nne wakati West Brom wao wamepanda mpaka nafasi ya 13 wakifikisha pointi 40.
UNAPASWA KUJUA KUWA......
- Ushindi walioupata West Brom ni ushindi wa kwanza kwa kocha Tony Pulis dhidi ya Manchester United akiwa ameshapoteza mara 10 na kutoka sare mara 1 tu.
- Hii ni mara ya kwanza Man United inapoteza mechi 3 mfululizo katika ligi kuu tangu mwezi Disemba mwaka 2001.
- Pia ni mara ya kwanza Manchester United inashindwa kufunga goli lolote katika mechi 3 mfululizo ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwezi May mpaka Agosti mwaka 2007.
No comments