LICHA YA KIWANGO CHA HALI YA JUU YANGA YATOLEWA TUNISIA


Wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa kutoka Tanzania na Afrka Mashariki na kati Yanga SC imeaga rasmi mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa bao 1-0 na Etoile Du Sahel ya Tunisia.

Yanga licha ya kufungwa bao hilo ilionyesha kiwango cha juu mno na kukosa nafasi kadhaa lakini ashukuriwe kipa wa Yanga leo Deo Munishi ambaye alijitahidi kuokoa michomo mingi iliyoelekezwa katika lango lake.

Etoile ambayo ilifanikiwa kuibana Yanga hapa nyumbani wiki mbilizi lizopita inavuka hatua hii ambapo sasa wataingia katika hatua ya mtoano ambayo itahusisha pia timu toka katika ligi ya mabingwa Afrika na washindi wa hapa wataingizwa katika makundi ya Kombe la Shirikisho.

Yanga wao watarudi nyumbani kuja kumalizia ligi ambayo tayari wameshatawazwa mabingwa hivyo kujiandaa na Ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.


No comments

Powered by Blogger.